COVID STATISTICS
https://www.worldometers.info/coronavirus/country/kenya/
LOCAL NEWS
ATWOLI ATAKIWA KUELEZA KUHUSU MKUTANO ULIOFANYWA NYUMBANI KWAKE WAKATI HUU AMBAPO TAIFA LINAKABILIANA NA JANGA LA CORONA
Shirika la moja la haki ya usawa na maendeleo limewaandikia barua ya makataa ya siku tatu waziri wa afya mutahi kagwe, waziri wa usalama fred matiangi na kiongozi wa mashtaka ya umma kuwakamata wanasiasa waliokusanyika kwenye boma la katibu wa cotu francis atwoli na kuwekwa kwenye karantini ya lazima kwa siku kumi na nne.
Wakiongea mjini kakamega mwenyekiti wa shirika hilo nchini bonface manda na afisa mkuu desterio okumu, wamezitaka wizara hizo kuharakisha mpango wa kuwaweka viongozi hao kwenye karantini kwa kukiuka amri ya serikali, kama njia moja ya kuwaonyesha wakenya kuwa taifa linaweka makali ya sheria hizo kwa mkubwa na mdogo.
Wanasema ni jambo la kushangaza kuona baadhi ya viongozi waliohudhuria kikao hicho wakirejea nyumbani na kutangamana na wananchi hata kwenye hafla za mazishi mashinani wakihofia kuwa huenda wakachangia kusambaa kwa virusi vya corona.
VIONGOZI KAUNTI YA KAKAMEGA WATOFAUTIANA KUHUSU KIONGOZI ATAKAYEPEPERUSHA BENDERA 2022
Wawakilishi wadi wa bunge la kakamega wametofautiana vikali kuhusu kiongozi ambaye ataongoza jamii ya waluhya kisiasa kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022.
Saa chache tu baada ya kundi moja likiongozwa na kiongozi wa walio wachache david ndakwa na walter andati kudai kuwa katibu mkuu wa miungano ya kutetea maslahi ya wafanyikazi nchini cotu francis atwoli na gavana wycliffe oparanya wanatumiwa na kinara wa chama cha odm raila odinga kugawanya viongozi wa jamii hiyo, sasa kundi lingine limejitokeza kuwatetea atwoli na oparanya.
Kundi hilo likiongozwa na kiongozi wa walio wengi bungeni humo joel ongoro, limepuuzilia mbali uongozi wa kinara wa anc musalia mudavadi na seneta moses wetangula wa ford kenya.
Awali kundi pinzani lilikuwa limedai kuwa francis atwoli na wycliffe oparanya ni vibaraka wa raila odinga ambao wanatumiwa kwa manufaa yake ya kibinafsi.
WAFANYIBIASHARA MJINI WEBUYE WAHIMIZWA KUTILIA MAANANI MASHARTI YA WIZARA YA AFYA
Kama njia mojawapo ya kukabiliana na janga la Korona katika kaunti ya Bungoma wafanyibiashara hasa kutoka mjini Webuye wamehimizwa kuzingatia masharti yaliyowekwa na wizara ya afya ikiwemo kunawa mikono,kuvalia barakoa na kukaa umbali wa mita moja wanapokuwa katika maeneo ya umma.
Akizungumza katika soko la Dina mjini Webuye baada ya kusimamia zoezi la kutangaza mshindi wa kura za viongozi wa soko hilo,afisa mkuu wa wizara ya biashara kaunti ya Bungoma Chris Simiyu amesema kuwa wafanyibiashara wako katika hali hatari ya kuambukizwa virusi vya Korona kutokana na kutangamana na watu wengi.
Kauli hiyo imeungwa mkono na kaimu mshirikishi wa serikali ya kaunti ya Bungoma katika eneo bunge la Webuye magharibi Eunice Simuli aliyewataka wafanyibiasahara hao kuzingatia masharti hayo ya wizara ya afya ikizingatiwa kuwa eneo la Dina linaunganisha vituo mbalimbali vya magari na hivyo kuhatarisha maisha yao ya kuambukizwa virusi vya Korona.
Nao baadhi ya viongozi waliochaguliwa akiwemo Roslyne Nambuye na Collins Mupalia wamepongeza kuteuliwa kwao na kuahidi kushirikiana na wafanyibiashara eneo hilo huku wakiwarai kuzingatia mashati ya wizara ya afya dhidi ya virusi vya Korona.
WAFANYIBIASHARA ENEO BUNGE LA MALAVA WAMEELEZEA KUATHIRIKA KWA BIASHARA ZAO KUTOKANA NA JANGA LA CORONA
Huku taifa likiendelea kupigana na janga la covid 19 baadhi ya wafanyibiashara wadogo wadogo katika eneo bunge la malava wameathirika pakubwa kutokana na kushuka kwa mapato yao.
Kwenye mahojianao na kituo hiki mjini malava wafanyibiashara hao wamehoji kuwa kwa sasa biashara ya imeathirika pakubwa tangu kuchipuka kwa virusi vya corona nchini wakidai kutengwa na serikali ya kitaifa na ile ya kaunti ya kakamega haswa wakati mgumu
Aidha wamemtaka rais uhuru kenyatta kulegeza kamba kuhusu masharti yaliyowekwa ili kurejelewa kwa shughuli za kawaida nchini wakiahidi kufuata maagizo ya wizara ya afya, jambo ambalo limeonekana kupingwa vikali na baadhi yao wakihofia kuenea kwa virusi hivyo mashinani.
NDERITU APONGEZWA KWA MSIMAMO WAKE DHABITI KUHUSU UAMUZI WA CHAMA CHA FORD KENYA
Msajili wa vyama vya kisiasa nchini Bi Ann Nderitu ametakiwa kuwa na msimamo dhabiti anapotoa uamuzi unaohusiana na mzozo wa vyama vya kisiasa nchini kama vile alivyo amua mzozo unaoshuhudiwa katika chama cha Fordkenya.
Akizungumza na wanahabari mjini Webuye mwanaharakati wa kisiasa kaunti ya Bungoma issack Wanjekeche amesema kuwa uamuzi wa Nderitu ulikuwa dhabiti na kumtaka kutoshawishika na viongozi wa kisiasa akisema kuwa idara ya usajili wa watu iko huru.
Wanjekeche hata hivyo ameutaka uongozi wa chama cha Fordkenya kuja pamoja na kutatua maswala yao ya kindani badala ya kukorofishana kila mara.
Bi Nderitu katika uamuzi wake ameutaka uongozi wa chama cha Fordkenya kutatua maswala yao kabla ya kuwasilisha makaratasi hayo huku akisema kwa sasa wanatambua Moses Wetangula kama kinara wa chama hicho
ATWOLI ASHUTUMIWA NA VIONGOZI WA CHAMA CHA ANC KWA MADAI YA KUWATAWANYA VIONGOZI WA MAGHARIBI
Wawakilishi wadi katika chama cha anc kaunti ya kakamega wamemshtumu katibu wa muungano wa wafanyikazi nchini francis atwoli kwa kile wanachodai anatumiwa kusambaratisha viongozi wa jamii ya mulembe.
Wakiwahutubia wanahabari mjini kakamega, wawakilishi wadi hao wakiongozwa na kinara wa wachache kwenye bunge hilo david ndakwa, wameapa kuwa kamwe hawatakubali kufanywa mnada kisiasa.
Wanahoji kuwa wao kama chama hawatakubali kuingia kwenye serikali kama wanavyodai viongozi wengine kutoka eneo hilo wakiongeza kuwa wako tayari kuunda serikali ifikapo mwaka wa 2022 chini ya kiongozi wao musalia mudavadi.
Kwa upande wake mwakilishi wadi wa isukha kusini farouk machanje amemtaka kinara wa odm raila odinga kuwa anayesewaskuma viongozi hao ili kujipatia umaarufu katika ukanda wa magharibi.
WASHUKIWA WA WIZI WANUSURIKA KIFO MJINI MALAVA KWA KUWATAPELI WAKAAZI
Washkiwa watatu wa wizi wa mpesa wameponea kifo baada ya wahudumu wa bodaboda kuwakimbiza kutoka eneo la navakholo hadi mjini malava ambapo walilazimika kukimbilia usalama wao kwenye kituo cha polisi cha kabras.
Watatu hao wanadaiwa kuwa miongoni mwa genge la watu ambao wamekuwa wakiwaibiwa wafanyibiashara wengi mjini malava kabla ya kufumaniwa waikijaribu kuwalaghai wakazi wa navakholo.
Kwa upande wake mzee jeremia ngaira amethibitisha kuwa mmoja wa washukiwa hao ni miongoni mwa washukiwa watatu ambao walimtembelea kwa boma lake aprili mwaka huu katika kijiji cha maramu na kumlaghai shilingi elfu kumi na tisa kutoka kwa simu yake.
Ni kisa ambacho pia kilimtendekea mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya samitsi peter masungo ambaye amedai kuwa aliibiwa zaidi ya shilingi elfu tano kwenye barabara ya malava samitsi.
tayari maafisa wa polisi wameanzisha uchunguzi kuhusiana na kisa hicho.
WANUFAIKIA NA BARAKOA NA SABUNI KULE BUTERE
Wakazi wa marama kaskazini eneo bunge la butere kaunti ya kakamega wamenufaika na msaada wa barakoa na sabuni kutoka kwa wakfu wa Jacob makanga
Jackson akhwale kutoka wakfu wa jacoba makanga amesema wanalenga kuchangia katika juhudi za kuwasaidia wakazi wa marama kaskazini kukabili changamoto za corona
Wakati uo huo wakfu huo ulikuwa katika kijiji cha mwiyenga kata ndogo ya inaya kutengeneza mto kuwawezesha wakazi kupata maji safi kama njia ya kuepuka maambukizi ya maradhi yanayotokana na maji chafu
Mwenyekiti wa wakfu wa makanga fanuel chamwoma na msimamizi wa maswala ya akina mama katika wakfu huo roda isomi wamesema ni mradi ambao unaendelezwa wadi nzima na wameitaka serikali kuekeza zaidi katika kutunza vyanzo vya maji kwani wakazi wengi hawawezi kumudu maji ya mifereji
MWANAFUNZI WA SHULE YA UPILI YA LUSUMU NAVAKHOLO AJIRUSHA KATIKA MTO LUSUMU
Biwi la simanzi limetanda katika kijiji cha kaunda kata ya lusumu eneo bunge la navakholo kaunti ya kakamega hii ni baada ya mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya upili ya st. kizito lusumu kujirusha ndani ya mto lusumu kwa madai ya kutofautiana na mamake kuhusu mimba.
Wanakijiji wakiongozwa na peter sikhore wanadai kuwa mwendazake wa miaka 17 alijirusha kwenye daraja ya lusumu baada ya kudaiwa kuwa na ugomvi na mamake mzazi kuhusiana na mimba ya miezi minne aliyokuwa nayo.
Hata hivyo mwili wa mwendazake uliondolewa na wanakijiji na kupelekwa nyumbani kwao, jamii ikisubiri maafisa wa polisi kufika bomani humo
RAILA ALAUMIWA KUHUSU MGOGORO UNAOSHUHUDIWA FORD KENYA
Huenda msukosuko ambao unashuhudiwa katika chama cha Ford Kenya unachochewa na kinara wa chama cha ODM Raila Odinga.
Ni kauli yake mchanganuzi wa maswala ya kisiasa katika kaunti ya Bungoma John Wanyama anayesema kuwa huenda kinara wa chama cha ODM Raila Odinga anatumia baadhi ya wanasiasa akiwemo mbunge wa Tongareni Eseli Simiyu,Mwenzake wa kanduyi Wafula Wamunyinyi na waziri wa ugatuzi Eugene Wamalwa kusambaratisha chama Fordkenya .
Wanyama amesema kuwa Chama cha Fordkenya huenda kikasambaratika zaidi kutokana na msukosuko ambao unazidi kushuhudiwa katika uongozi wa chama hicho hali hiyo ikichangiwa na ubinafsi mingoni mwa wanachama wa chama hicho .
Kuhusiana na swala la vigogo wa kisiasa eneo la magharibi Musalia Mudavadi na Moses Wetangula kutohudhuria mkutano ulioandaliwa na katibu mkuu wa COTU Francis Atwoli nyumbani kwake kaunti ya Kajiado Wanyama amekuwa na haya ya kusema.
ASKOFU KHAMALA AKASHIFU MGOGORO UNAOENDELEA KATIKA CHAMA CHA FORD KENYA
Mbunge wa lurambi Askofu Titus khamala amekashifu mgogoro ambao unazidi kushuhudiwa kwenye chama cha ford Kenya akisema unalenga kuchokora uthabiti wa jamii ya waluhya kuungana nyuma ya kiongozi wa ANC Musalia mudavadi na mwenzake wa ford Kenya moses wetangula mbele ya uchanguzi wa mwaka Elfu mbili ishirini na mbili
Mgogoro unaoshuhudiwa kwenye chama cha Ford Kenya ni kizingiti ambacho kinalenga kusambaratisha jamii ya Mulembe kutoingia Ikulu kupitia kwa kinara wa ANC Musalia Mudavadi itimiapo mwaka 2022.
Ni matamshi Yake mbunge wa lurambi bishop Titus Khamala Akisema mvutano unaoshuhudiwa kwenye chama hicho ni vita kutoka jamii zingine ambazo zinalenga kusambaratisha kura za waluhya jambo ambalo anasema halitawezekana Kamwe kutokana na msimamo dhabiti ulioko kwa sasa.
Akiongea alipozindua ujenzi wa nyumba za polisi katika eneo la matioli wadi ya butsotso kusini na pia ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi ya emukaba. bustsotso mashariki,Bishop khamala amesema jamii ya waluhya iko nyuma ya kinara wa ANC musalia mudavadi ambaye hana ubaya wowote na serikali ya jubilee lakini hawatakubali hatua ya kuvuruga vyama vya kisiasa kwa sasa.
WAKAAZI WA MALAVA WAJIVUNIA SERIKALI ZA MAGATUZI NCHINI SIKU KUU YA MADARAKA
Huku taifa likiadhimisha miaka 57 ya siku kuu ya madaraka wakaazi wa eneo bunge la malava wanajivunia kubuniwa kwa serikali za magatuzi nchini.
Wakizungumza na kituo hiki wakaazi hao wameleza kujivunia kuwepo kwa nafasi za kazi miongoni mwa wamama na vijana na kuzinduliwa kwa miradi mbali mbali ya maendelo mashinani.
Hata hivyo wakaazi hao wamesikitikia namna sherehe za madaraka mwaka huu zilivyoendeshwa kufuatia kuwepo kwa janga la corona wengi wakilazimika kuitazama sherehe hiyo kupitia kwenye runinga.
Hidha wameirai serikali ya kitaifa kuongeza mgao wa fedha kwenye serikali ya kaunti ya kakamega ili kufanikisha miradi zaidi ya maendeleo eneo hilo..
WAHUDUMU WA BODA BODA WADAI KUHANGAISHWA NA BAADHI YA WANASIASA ENEO HILO
Wahudumu wa bodaboda kutoka mjini Webuye wamewataka wanasiasa eneo hilo wanaoingilia maswala yao ya kindani kujitenga nayo na badala yake kuwahudumia wakaazi waliowachagua.
Wakizungumza na wanahabari mjini Webuye wahudumu hao wa bodaboda wakiongozwa na Mwenyekiti wao Milton Maloba na Stephen Owino wamedai kuwa baadhi ya viongozi eneo hilo akiwemo mwakilishi wadi ya Matulo Paul Wanyonyi amekuwa akishirikiana na baadhi ya vijana kusambaratisha sekta ya bodabodo eneo hilo.
Wahudumu hao wa bodaboda hata hivyo wameitaka idara ya usalama eneo hilo kuingilia kati na kuwalinda baada yao kupokea vitisho kutoka kwa baadhi ya wahudumu wenzao.
Hata hivyo wamewataka viongozi wa kisiasa kuwapa misaada wakti huu wa janga la Korona badala ya kujihusisha na mambo yasiyofaa.
MZOZO WA SHAMBA WAZUKA BAINA YA JAMII ZA WALUHYA NA WANANDI MPAKANI IKOLI May 30, 2020
Kumeshuhudiwa mzozo wa shamba kati ya jamii zinazoishi mpakani mwa waluhyia na wanandi katika eneo la Ikoli eneo bunge la Malava kaunti ya Kakamega usiku wa kuamkia leo huku wengi wa wakaazi hao wakiachwa na majeraha mabaya.
Kulingana na baadhi ya wakaazi wa Ikoli inasemekana mzozo huo ulizuka kati ya familia mbili ikiwemo ile ya Samwel na ile ya Angasi na kisha kusababisha vita vya jumla kati ya wakaazi wa jamii hizo mbili.
Aidha wanasema ni mgogoro ambao umekuwepo kwa muda sasa huku juhudi za kuleta amani kati yao zikiambulia patupu na sasa wanaiomba serikali kuu kuingialia kati na kuleta suluhu la kudumu na kukomesha mzozo huo wa mara kwa mara.
SOKO MJINGA WEBUYE YAKESHA NJE YA KIJIBARIDI BAADA YA MVUA KUNG’OA PAA 29/5/2020
Zaidi ya jamii kumi kutoka kijiji cha soko Mjinga wadi ya matulo eneo bunge la Webuye maghribi zimelazikia kukesha kwenye kijibaridi kali baada ya nyumba zao kubomolewa na mvua nyingi iliyoshuhudiwa eneo hilo hivi majuzi.
Wakizungumza na wanahabari jamii hizo zikiongozwa na Judith Wafula na Moses Juma wamesema kuwa mvua hiyo iliyonyesha siku ya alhamisi ilibomoa nyumba zao na kuharibu kila kitu wanachomiliki huku wakihangaika na kulazimika kulala kwa kibaridi kikali.
Wathiriwa hao hata hivyo wamewataka wahisani wakiwemo mwakilishi wadi wa eneo hilo Paul Wanyonyi na mbunge Dan Wanyama kujitokeza na kuwasaidia ili wakarejerejelee maisha yao ya kawaida.
FORD KENYA YAUNGA MKONO UTEUZI WA ESELI KAMA NAIBU KIRANJA BUNGENI 29TH May 2020
Chama cha Ford Kenya kaunti ya Bungoma kimeunga uteuzi wa mbunge wa Tongaren kama naibu wa kiranja katika bunge la kitaifa
Haya ni kwa mjibu wa katibu wa chama hicho kaunti ya Bungoma Cephas Wachana
Kwa mjibu wa Wachana amepongeza muheshimiwa Eseli simiyu kwa kupewa nafasi hiyo na bunge la kitaifa huku akisema chama cha Ford Kenya kiko imara
Hata hivyo amepuzilia mbali madai kuwa kuteuliwa kwa muheshimiwa eseli ni kusaliti chama cha Ford Kenya akisema chama kiko imara
MBUNGE MALULU INJENDI ANYOSHA MKONO WAKE KWA WAKAAZI WA ENEO BUNGE LA MALAVA 29TH May 2020
Familia zisizojiweza kutoka eneo bunge la Malava zimenufaika kutokana na msaada wa chakula wa zaidi ya magunia 200 ya mahindi, barakoa pamoja na sabuni ya kunawa mikono kutoka kwa mbunge wa eneo hilo Malulu Injendi kama njia mojawapo ya kuthibiti maambukizi ya virusi vya corona nchini.
Akizungumza mjini Malava punde tu baada ya kutoa msaada huo, mbunge huyo amepongeza kamati maalumu iliyobuniwa kusimamia mpango huo ukiongozwa naye naibu kamishna wa eneo hilo Simon Kobia akiwataka wakazi kuendelea kuzingatia maagizo yaliyotolewa na wizara ya afya katika kukabili janga la corona nchini.
Aidha Malaulu ametumia fursa hiyo kuitaka serikali ya kitaifa kuangazia wanainchi wasiyojiweza sehemu zote za mashinani kama inavyofanya kwa wahanga wa mafuriko kote nchini.
Kwa upande mwingine Malulu amewarai wafuasi wa chama cha Jubilee kutotishwa na mgogoro unaoendelea chamani humo akisema chama hicho kingali imara.
AFISA SIMON LOKORIO ATOA WITO KWA WAKAAZI WA MATETE KAUNTI YA KAKAMEGA 29th May 2020
Naibu kamishna wa eneo la Matete kaunti ya Kakamega Simon Lokorio ameelezea hofu yake kuwa huenda virusi vya corona vikaenea eneo hilo baada ya kubainika kuwa wengi wa wakazi wa eneo hilo wanapuuzilia mbali maagizo ya wizara ya afya ya kujikinga dhidi ya virusi hivyo.
Akizungumza na wanahabari katika eneo hilo, Lokorio amesema kuwa licha ya serikali na mashirika mengine kusisitiza umuhimu wa kufuata maagizo hayo, wakaazi wengi wanaendelea kuishi kama kawaida.
Aidha Lokorio amewaonya wakaazi wa eneo hilo kuwa huenda ugonjwa huo wa covid 19 ukasambaa miongoni mwao na kusababisha maafa.
Kuhusu mvua nyingi inayoendelea kushuhudiwa eneo hilo, naibu kamishna huyo amewatahadharisha wenyeji dhidi ya kuogelea mitoni na kutumia daraja zilizo katika hali duni kama njia mojawapo ya kuepuka kusombwa na maji.
SUMBI ATETEA WAFANYIKAZI WA KAUNTI 29/5/2020
Afisa mkuu wa wafanyikazi kaunti ya kakamega Robert Sumbi amejitokeza kumtetea gavana wa kaunti ya kakamega Wycliffe Oparanya kutokana na tuhma za ufisadi zinazozidi kutolewa na baadhi ya viongozi
Sumbi amewasuta wanaomkashifu gavana akiwataja kama wenye nia fiche akiwataka kufika mbele ya vitengo vya sheria kuwasilisha ushahidi wao kuhusu baadhi ya maafisa wa kaunti hiyo kuchunguzwa na tume ya kupambana na ufisadi
Sumbi aidha amewatahadharisha baadhi ya viongozi wanaotumia swala la corona kujipa umaarufu wa kisiasa akiwataka kufwata njia mwafaka za kuwasaidia wakaazi maeneo tofauti
Kuhusu swala la kufunguliwa kwa shule kiongozi huyo ameitaka wizara kuweka mikakati ya kutosha ili kuzuiya kuenea zaidi kwa virusi hivyo vya corona miongoni mwa wanafunzi
VIONGOZI WA KANISA WAJITOKEZA KUSAIDIA WAJANE WAKATI HUU WA JANGA LA CORONA 29/5/2020
Viongozi wa makanisa kutoka eneo la Butere akiwemo kasisi wa kanisa la Miracle Butere wanakashifu hatua ya serikali kubomoa makao ya wakaazi wakisema kuwa familia nyingi huenda zikashikwa na magonjwa ya Malaria kwa kulala kwa baridi
Ni kauli yake kasisi wa kanisa hilo Ibrahim Makokha ambaye amesema wakati huu wa janga la corona na mafuriko sio wakati mzuri wa serikali kubomoa makao ya wakaazi na hii ni baada tu ya nyumba kadhaa kubomolewa kule Kariobangi ikidaiwa kuwa ni shamba la serikali
Vilevile kiongozi huyo amesema walinda usalama waangazie maswala ya usalama wakati huu wa kutekeleza Curfew kwani vijana wengi wamejiingiza kwa tabia za kuvunja nyumba wakati wa usiku na kuiba
Viongozi hao walikuwa wameandamana na msaidizi wa aliyekuwa mbunge wa Butere Andrew Toboso wakati wa kupeana msaada wa vyakula kwa walemavu na mama wajane kutoka wadi ya Marama South na kusihi viongozi wengine kujitokeza na kusaidia wakaazi wa butere
MIPANGILIO YA KUPIGANA NA JANGA LA CORONA ENEO BUNGE LA MATUNGU NA BUTERE 29/5/2020
Huku nchi ikizidi kupigana na janga la corona baadhi ya viongozi kutoka serikali kuu wakiwemo naibu kamishina wanazidi kufanya mikakati kuhakikisha uenezaji wa janga hilo mashinani imekoma
Wakizungumza na wanahabari DC wa Butere Elias Kithaura na mwenzake wa Matungu Jacob Awuor wamesema wameweka mipangilio kabambe kuona kuwa wakaazi wameepukana na kuambukizana kwa ugonjwa huo huku kupima joto mwilini kwenye barabara kuu ikiwa moja ya mipangilio hiyo
Aidha viongozi hao wamesema serikali kuu imeanza mipango ya kuwalipa familia zisizojiweza pesa kidogo wakati huu wa janga la corona kuona kuwa wamejimudu maishani na haya ni majina ambayo yaliwasilishwa kwenye afisi yao kupitia kwa machifu
WAZIRI BARAZA WANGWE AWATAKA WAKAAZI KAKAMEGA KUZINGATIA MAAGIZO YA WIZARA YA AFYA 29/5/2020
Waziri wa maji na mazingira kaunti ya Kakamega Baraza Wangwe amewataka wenyeji wa kaunti hiyo kuzingatia masharti ya wizara ya Afya ikiwemo ya usafi kama njia pekee ya kukabiliana na kuenea Kwa virusi vya corona.
Akizungumza kwenye hafla ya kukagua miradi ya maendeleo haswa maji inayotekelezwa na serikali ya kaunti hiyo eneo bunge la Navakholo Wangwe amesema kuwa kama serikali wametanga zaidi ya shilingi milioni kumi kufanikisha miradi ya maji eneo bunge la Navakholo na kuhakikisha kuwa kuna maji ya kutosha kupiga jeki vita dhidi ya ugonjwa wa corona
Kauli ya Wangwe iliyoungwa mkono na Mwakilishi wadi wa Bunyala ya Kati Ben Samba Wanzofu aliyeonyesha kuridhika kwake na jinsi wakazi hao wanavyokumbatia masharti hayo.
WAZAZI WATAKIWA KUWACHUNGA WANAO KAUNTI YA BUNGOMA 29/5/2020
Kama njia mojawapo ya kukabiliana na jangaa la korona vijijini wazazi katika kaunti ndogo ya Webuye magharibi wamehimizwa kuwalinda wanao na kuwazuia kutembea kila mara katika maeneo yaliyo na watu wengi.
Akizungumza na wanahabri mjini Webuye msaidizi wa naibu kamishna kaunti ndogo ya Webuye magharibi Penina Kuto amesema kuwa kuna baadhi ya wazazi ambao wamekuwa wakiwaruhusu wanao kurandaranda katika sehemu mbalimbali ikiwemo eneo la Dina mjini Webuye na hivyo kuhatarisha maisha yao .
Kauli hiyo imeungwa mkono na mwenzake wa Bokoli Chitechi Marystella aliyewataka wazazi kuzinagtia elimu ya wanao hasa wakti wakiwa nyumbani huku akiahidi kushirikiana na wakaazi wa eneo hilo kupanda miti kama njia mojawapo ya kulinda mazingira.
WAKAMATWA KW KUKOSA KUFUATA MAAGIZO YA SERIKALI KUHUSU KUFUNGUA HOTELI KULE MUMIAS 29/5/2020
Polisi mjini Mumias kwa ushirikiano na maafisa wa afya ya umma wamewakamata wamiliki 11 wa mikahawa katika mji wa mumias kwa kukosa kufuata maagizo ya serikali katika juhudi za kupambana na janga la COVID 19 nchini.
Akizungumza na wanahabari baada ya msako huo, OCPD Mumias Paul Kipkorir amesema kuwa wataendelea na msako huo kuhakikisha hakuna mkahawa unaendelea kutoa huduma ya kupika na kuuza vyakula pasi na kufuata masharti ya serikali.
Korir amesema 11 hao watafikishwa mahakamani hapo kesho huku akitoa tahadhari kwa wakaazi ambao hawazingatii maagizo yanayotolewa na serikali katika kupambana na virusi vya corona nchini
KIWANDA CHA SAMAKI CHA TARAJIWA KUFUNGULIWA WIKI MBILI ZIJAZO KAUNTI YA KAKAMEGA
Serikali ya kaunti ya kakamea kupitia wizara ya biashara na viwanda imo mbioni kuchimba visima elfu 30 kwa wakulima wao ili kukithi kiwango hitaji cha tani saba ya samaki kila siku kwa kiwanda samaki ambacho kinanuiwa kufunguliwa kwa muda wa wiki mbili zijazo.
Ni kauli ya waziri wa biashara kaunti hiyo ya kakamega Kassim Were ambaye amesema kuwa wameweka mikakati ya kutosha kufufua kilimo cha samaki eneo hilo kama njia moja ya kuinua uchumi wa kaunti hiyo.
Hata hivyo wakulima wakiwakilishwa na mwenyekiti wao Laban Mwanzo wameitaka serikali hiyo kuwasaidia kifedha ili kufanikisha mradi huo .
MIMBA ZA MAPEMA KATIKA KAUNTI YA KAKAMEGA 21/5/2020
Mimba za mapema kwa watoto wasichana zimetajwa kuwa changamoto kubwa kwa jamii hasa wakati huu wa janga la corona ambapo wanafunzi wamesalia nyumbani kwa mda mrefu, ni kauli yake mshirikishi wa shirika lisilo la kijamii actionaid pauline atieno na mwenzake wa khwisero Pambazuko Chapter Grace Sande
Pauline na mwenzake wa shirika la kwisero Pambazuko Chapter Grace Sande wamesema idadi kubwa ya watoto wasichana wamepachikwa mimba na wengine 15 kupotea ikiwa changamoto kubwa kwa jamii
Aidha wametaka wazazi kukaa na wanao hasaa wakati huu wa janga la corona na pia janga la mafuriko
Walikuwa wakizungumza haya wakitoa msaada wa visodo na vyakula kwa familia zinazoishi katika shule ya singi ya mushiangubu eneo bungee la khwisero
MWANAMKE MWENYE UMRI WA MIAKA 34 AUWAWA NA MPENZI WAKE KISHA MWILI WAKE KUPELEKWA KATIKA HIFADHI YA MAITI YA KAKAMEGA 20/05/2020 STORY BY BELLBUT PHERRILAH
Polisi mjini Kakamega wanachunguza kisa cha mauaji ya mwanamke wa umri wa miaka 34 anayedaiwa kuuliwa na mpenziwe ambaye ni afisa wa polisi wa utawala kisha kuupeleka mwili wake katika hifadhi ya wafu ya hospitali ya rufaa ya kakamega.
Inadaiwa kuwa marehemu ,Elizabeth Migedi ambaye hufanya kazi vyungani mwa mji wa kakamega, alionekana mara ya mwisho akiandamana na mpenziwe ambaye ni afisa wa polisi, kabla ya kupatikana ameuawa kiunyama.
Ikiongozwa na nduguye Joseph Isechi familia ya mwendazake inalilia haki kwa serikali ,kwani wanaelezea dada yao amekuwa akizozana na mpenziwe kila mara na huenda sababu kuu ya kupelekea kutokea kwa kifo chake.
David Kabena ambaye ni OCPD wa Kakamega , amedhibitisha mauaji hayo na uchunguzi umeanzishwa kubaini kilichopelekea mauaji hayo.
Mwili wa mwendazake kwa sasa umepelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya rufaa ya kakamega ambapo unatarajiwa kupasuliwa ili kiini cha kifo chake kikabainike wazi
BAJETI YA ZIADA YALETA UTATA KAUNTI YA KAKAMEGA JE KUNA NINI? 20/05/2020 STORY BY BELLBUT PHERILLAH
Hali ya malumbano yanazidi kushuhudiwa kwenye bunge la kaunti ya Kakamega kutokana na kuibuka kwa madai ya kuongezeka kwa fedha kupitia mlango wa nyuma.
Hii ni baada ya mwakilishi wadi wa Butsotso kusini Wolta Andati miongoni mwa wengine kuweka wazi maoni yao jinsi bajeti hiyo imepotokwa bila kujali wakaazi wa mji wa huo hasa wakati huu mgumu wa janga la Corona.
Hali ya vute ni kuvute imeonekana kuenea katika bunge la Kakamega baada ya miongoni mwa wawakilishi wadi Kwenye serikali hiyo kuonekana kutofautiana vikali namna bajeti ya ziada, iliopitishwa juma moja lililopita iliweza kuendeshwa na wawakilishi hao.
Upande wa wengi ukionekana kutofautiana na mwenye kiti wa bajeti hiyo Willis Opuka waliposema kuwa, pesa hizo zinatumika kuwezesha klabu ya Kakamega home boys na hivyo basi Opuka akidai ni pesa zinazowalipa wachezaji kutoka kaunti ya kakamega wanaosakata soka katika ligi kuu nchini tofauti na mshahara wanaolipwa na vilabu hivo.
MASHIRIKA YALETA MSAADA KWA WAATHIRIWA 20/5/2020
Waathiriwa wa mafuriko eneo bunge la Khwisero na wanaoishi katika shule ya msingi ya Mushiangubu hivi leo wamenufaika na msaada wa dawa, blanketi na mchele kutoka kwa shirika la Uhai Community Empowerment na Living Water
Wakizungumza na wanahabari baada ya kupeana msaada huo Jim Raul kutoka kwa shirika la living water na mwenzake wa uhai cef moses amakobe wamesema walionelea kutoa msaada kwa waathiriwa hao kwa kurudisha mkono kwa jamii kwan jamii nyingi zimekuwa zikihangaika wakati huu wa mafuriko
Kulingana na Moses Amakobe amesema kuwa serikali inafaa iweke suluhuya kudumu kwenye mito hiyo kuona kuwa wakaazi wanaoishi kando ya mito hawaathiriki tena
Chief wa eneo hilo Paul Ambaisi amepongeza mashirika hayo kwa kuleta msaada kwa waathiriwa na ametoa wito kwa waahisani kujitolea na kujenga nyumba kwa waathiriwa hao kwani wengi wao nhumba zimebomoka
Walioathiriwa walishukuru msaada huo
JAMAA (32) AMUOA MWANAFUNZI WA MIAKA KUMI NA MITANO KAUNTI YA KAKAMEGA ENEO BUNGE LA KHWISERO
Polisi mjini Kakamega wanamzuilia mwanamme wa miaka 32 kutoka kijiji cha Shivakala eneo bunge la Khwisero baada ya kufumaniwa akiwa amemuoa na mtoto wa miaka 15.
Chifu wa kata ya Bukhungu Maurice Muchiti amesema mshukiwa Gilbert Shikondi alifumaniwa na wananchi kabla kukabidhiwa kwa wazee wa mtaa, ambapo baada ya kufikishwa afsini mwake, alidai kuwa mwanafunzi huyo alikwama ndani ya nyumba yake akisema anataka kuolewa kwake.
Ocpd wa Kakamega David Kabena amehoji kuwa mshukiwa atafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kuakamilika.
mwisho
MASHIRIKA YA MIKOPO KAUNTI YA BUNGOMA YAONYWA DHIDI YA KUWAHANGAISHA WADENI WAKE
Mashirika mbalimbali ya mikopo ambayo yanakiuka amri ya serikali na kuwalazimisha wafanyibiashara hasa wahudumu wa bodaboda kulipia madeni yao ya mikopo ya pikipiki wakti huu taifa linapambana na janga la korona yatachukuliwa hatua za kisheria.
Haya ni kwa mujibu wa afisa mkuu mtendaji wa muungano wa wafanyibiashara [chambers of commerce] kaunti ya Bungoma Patrice Chenge,anayesema kuwa kwa sasa wafanyibiashara wanapitia hali ngumu ya maisha na sio vyema kwa mashirika hayo kuwatoza fedha huku akiwataka wale wote wanaotozwa fedha hizo kuripoti maramoja kwa afis zao.
Ni hivi majuzi ambapo wahudumu wa bodaboda mjini Webuye kupitia mwenyekiti wao Milton Maloba walilalamikia kunyanyswa na mashirika ya mikopo wakidai kunyanganywa pikipiki zao na kuitaka serikali kuingilia kati na kuwanusuru kutokana na hali hiyo.
MULUKA ATAKA COTU KUWAJIBIKIA SWALA LA WAFANYIKAZI WAKATI WA CORONA
Katibu mkuu wa chama cha ANC Barack Muluka ameyataja malumbano ya kisiasa yanayoendelea nchini kua yasiyofaa.
Akizunguma na wanahabari katika eneo bunge la Khwisero Muluka amesema kua viongozi wote wakiwemo rais Kenyatta kwa sasa wanafaa kuwa wakishughulikia masuala ya athatri za janga la corona badala ya kujihusisha na siasa za mwaka wa 2022.
Muluka pia amekashifu hali ya katibu mkuu wa cotu francis atwoli kujiingiza katika siasa za mwaka wa 2022 badala ya kushughulikia maslahi ya wafanyakazi nchini wakati nchi inazidi kupigana na janga la corona
Aidha muluka amesisitiza kuwa chama cha ANC bado kiko katika muumgano wa NASA na wala hawana mpango wowote wa kujiunga na muungano mwingine.
AFISA WA POLISI KAKAMEGA AONYESHA UTUMISHI WAKE KWA KUKARABATI UWANJA
Afisa mmoja wa polisi anayehudumu katika kituo cha matete amejitokeza na kuanza kuukarabati uwanja wa michezo wa kaunti ndogo ya matete kwa ushirikiano na wenyeji wa eneo hilo, kama njia moja ya kukuza vipaji miongoni mwa wakazi wa eneo hilo.
Afisa huyo anayefahamika kama Moses Mang’eni amehoji kuwa aliamua kufanya hivyo baada ya kugundua kuwa uwanja huo umekuwa ukitumika kwa wingi wakati wa hafla mbalimbali katika eneo hilo licha ya kuwa katika hali mbovu.
Ni juhudi zilizopokelewa vyema na wenyeji wa eneo hilo wakimtaka gavana wa kaunti ya kakamega Wycliffe Oparanyakuweka mikakati ya kuanza kukarabati uwanja huo.
VIONGOZI WA KIDINI WAZIDI KUSHINIKIZA KUFUNGULIWA KWA MAKANISA-ABDI SWALEH NI MWENYEKITI WA MAIMAMU KANDA YA MAGHARIBI
Mwenyekiti wa baraza la maimamu kanda ya Magharibi Abdi Swaleh ameitaka serikali ya kitaifa kuweka mikakati maalumu kwenye maeneo yote ya kuabudu kama inavyofanyika katika sehemu za mikahawa na burudani nchini.
Akizungumza na kituo hiki mjini malava, mwenyekiti huyo amehoji kuwa ni misikiti pamoja makanisa pekee yatakayowaunganisha wakenya haswa taifa linapopigana na virusi hatari vya corona.
Aidha Swaleh ametumia fursa hiyo kuwashauri wazazi wote nchini kuhakikisha watoto wao wanafuata maadili mema wakiwa makwao haswa wakati huu ambapo shule zote nchini zimefungwa.
TIBA YA UGONJWA WA CORONA YAMJIA NDOTONI MWANAFUNZI MMOJA KAUNTI YA BUNGOMA
Daktari Isaac Michael misiko amejitokeza kutetea tiba ya asili kwa ugonjwa wa Corona.
Haya yanajiri wakati ambapo baadhi ya wananchi wamezidi kushtumu mwanafunzi wa shule ya upili ya Kisioyi anayedai aliota ndoto na kufasiriwa tiba ya Corona.
Mwanafunzi huyo kwa jina Naomi Nafula alipelekwa kwa Misiko na mwalimu mkuu wa shule hiyo Robert Mang’oli ambaye aliomba serikali kutilia maanani ndoto hiyo.
Hata hivyo, baadhi ya wananchi wamezidi kuikemea ndoto hiyo wakidai ni utapeli huku Misiko akisizitiza kuwa pana haja ya uchunguzi zaidi kufanywa ili kuimarisha dawa hizo jinsi nchi ya Madagascar ilivyofanya.
SERIKALI KUU NA ILE YA KAUNTI YA KAKAMEGA ZATAKIWA KUFUATILIA MISAADA INAYOTOLEWA KWA WATU WASIOJIWEZA
Baadhi ya wakazi wa eneo la navakholo kaunti ya kakamega wamelalamikia ubaguzi katika idara ya fedha za walemavu na wazee huku wale wanaostahili wakiachwa nje
Wakiongozwa na mildred luvisia wakaazi hao wanasema wanafaa kufaidika kutokana na misaada hiyo ya serikali, na kinyume cha matarajio kupata kuwa kila mara wanasazwa nyuma licha ya juhudi za familia walio nazo.
Hayo yanajiri huku wakiitaka serikali kuu na ile ya kaunti ya Kakamega kuhakikisha kuwa , miradi inayolenga wenye changamoto kote nchini inawafakia pasipo kuwanufaisha wasiostahili.
WENYEJI WA KAUNTI YA BUNGOMA WANUFAIKA NA MISAADA YA CHAKULA
Serikali ya kaunti ya Bungoma kwa ushirikiano na shirika la msalaba mwekundu pamoja na muungano wa wafanyibiashara kaunti ya Bungoma umeanza kusambaza chakula cha msaada kwa wakaazi wa eneo hilo kama njia mojawapo ya kuwanusuru wakti huu mgumu wa janga la Korona na mafuriko.
Akizungumza baada ya kuzuru maeneo mbalimbali ikiwemo kambi ya waathiriwa wa janga la mafuriko la Mukite eneo bunge la Webuye magharibi na wadi ya maeni eneo bunge la Kimilili,waziri wa maji na mazingira katika kaunti ya Bungoma Renson Makheti amesema kuwa serikali ya kaunti ya Bungoma na mashirika mengine yameshirikiana ili kuwanusuru wahanga hao wa mafuriko na Korona hasa wakti huu wanapopitia hali ngumu ya maisha
Waziri makheti hata hivyo amewataka wakaazi wanaoishi sehemu zilizoathirika na mafuriko kuhamia mahali salama ili kuepuka kusombwa na maji hasa wakti huu ambapo taifa linashudia mvua nyingi kauli iliyoungwa mkono na afisa mkuu mtendaji wa muungano wa wafanyibiashara kaunti ya Bungoma Patrice Chenge.
Nao baadhi ya wakaazi walionufaika na msaada huo wamepongeza serikali ya kaunti ya Bungoma kwa kujitolea kwake kuhakikisha kuwa hawaangamizwi na njaa wakti huu mgumu wa janga la Korona na mafuriko.
BAADHI YA VIONGOZI WAPINGA KAULI YA MBUNGE WA KHWISERO YA WAKAAZI KUTAFUTA TITLE DEEDS
Baadhi ya viongozi kutoka eneo bunge la khwisero wamepinga hatua ya mbunge wa eneo hilo christopher aseka ya kusema kuwa wakaazi walioathirika na mafuriko kufanya mikakati ya kutafuta stakabadhi za kumiliki shamba ukipenda title deeds ndiposa wahamishwe mahali salama
Ni kauli yake mkuu wa sheria kaunti ya kakamega na tena kiongozi kutoka eneo la khwisero moses sande ambaye ametofautiana vikali na usemi wa mbunge wa eneo hilo kwani kulingana na sheria yeyote anayeishi kando ya mto hasa mito mikubwa inaonekana kuwa mali ya serikali basi hivo itakuwa vigumu kupata stakabadhi za kumiliki mashamba kama hayo
Ni kauli iliyoungwa mkono na mwakilishi wa wadi eneo la kwisero gofrey ommatera akisema kuwa itakuwa vyema mbunge wa eneo hilo kuwasilisha mjadala wa stakabadhi za mashamba bungeni kuona kuwa waathiriwa hao wamepata stakabadhi hizo kwa njia ya haraka
WAKAAZI WA MATUNGU ENEO LA NAMUTENDA WALALAMIKIA BARABARA MBOVU
Wakaazi wa eneo la namutenda eneo bunge la matungu katika wanalalamikia ubovu wa barabara inayounganisha maeneo ya mulwanda na mirere.
Barabara hio haijaweza kupitika kwa muda wa miezi minne baada ya kukatika na kulingana na wakaazi wa kijiji cha namutenda hakuna hatua yeyote iliyochukuliwa na viongozi wao
Wenyeji wanadai kuwa wamekua wakipitia masaibu mengi na sasa wanalazimika kulipa ada ya shilingi ishirini kwa vijana waliojitolea kuirekebisha barabara hio ndipo wapite,
Sasa wanatoa wito kwa mbunge wa matungu ajustus murunga aingilie kati tatizo hilo na kutoa suluhu ya kudumu.
Juhudi za kufikia chifu wa eneo hilo kuzungumzia swala hilo Edward Rapando ziliambulia patupu kwani alidinda kushika simu zetu
WAPOTEZA MAISHA WAKIJARIBU KUOKOA MASAA YA KAFYU KULE KAUNTI YA KAKAMEGA
Siku moja baada ya mhudumu wa bodaboda na abiria wake wawili kupoteza maisha kwenye barabara kuu ya kakamega kisumu karibu na kituo cha kibiashara cha shirere akiokoa maasa ya kafyu, mhudumu mwingine wa pikipiki amefariki baada ya kuruka maduka na kushindwa kudhibiti pikipiki usiku wa kuamkia leo.
Kulingana na walioshuhudia ajali hiyo marehemu aliyekuwa akitoka sehemu ya khayega kuelekea kakamega, aliruka maduka kwa mwendo wa kasi akijaribu kuokoa masaa ya kafyu akihofia kukutana na maafisa wa polisi na hivyo basi kusababisha pikipiki aliyokuwa akiendesha kukosa mwelekeo na kutumbukia ndani ya mtaro kupelekea kifo chake.
Hii inajiri siku moja tu baada ya mhudumu wa pikipiki aliyekuwa amewabeba watu wawili kufariki eneo hilo alipoingia kwenye trela iliyokuwa ikitoka kituo cha biashara cha shirere, huku abiria wake wakifariki walipokuwa wakiendelea na matibabu katika hospitali ya rufaa ya kakamega.
Ocpd wa shinyalu robert makau amewataka wahudumu wa pikipiki kusitisha kuendesha pikipiki zao mwendo wa kasi wakihofia kutiwa mbaroni na maafisa wa polisi ili kuzuia maafa kutokea kila mara.
IDADI YA WAGONJWA WANAOTAFUTA MATIBABU KATIKA HOSPITALI NDOGO YA MALAVA KAUNTI YA KAKAMEGA YAPUNGUA
Idadi ya wagonjwa wanaojitokeza kutafuta huduma ya afya kwenye hospitali ya malava kaunti ya kakamega inazidi kupungua huku wakazi wengi wakiendelea kuvumilia machungu ya maradhi mbalimbali kwa kuhofia kupimwa au hata kuambukizwa virusi vya corona.
Kulingana na fred amudavi ambaye ni afisa mkuu wa afya ya uma kaunti ndogo ya malava ni kuwa idadi ya wagonjwa waliokuwa wakitibiwa hospitalini humo hapo awali imerudi chini akihofia kuwa huenda hali hiyo ikasababisha athari kubwa miongoni mwao.
Aidha amudavi amewahakikishia wakazi hao usalama wa kutosha akisema kuwa tayari mikakati maalumu imewekwa kwenye hospitali hiyo ili kuzuia uambukizwaji wa virusi hivyo.
Vilevile afisa huyo amewashauri wenyeji kujitokeza nakutoa habari kwa wahudumu wa afya kuhusu wenzaoambao wamesafiri kutoka maeneo yaliyoathirika kamanjia moja wapo ya kuzuia kusambaa kwa ugonjwa wacovid 19.
1.NGARIBA KATIKA KAUNTI YA BUNGOMA WATOA KAULI YAO WAKTI HUU WA JANGA LA CORONA
Wapashaji tohara kaunti ya Bungoma wanataka wizara ya utamaduni kaunti hiyo kutoa mwelekeo kuhusu upashaji tohara kufuatia ongezeko la ugonjwa wa Covid 19 nchini
Kwenye kikao na wanahabari wakiwa Nalondo eneobunge la Kabuchai wakiongozwa na mwenyekiti wao Sinino Mkolongolo wamesema licha yao kusitisha shughuli za upashaji tohara hadi janga la korona litakapokabiliwa wanasema baadhi ya watu na hospitali zinaendeleza zoezi hilo wanalosema ni kinyume na utamaduni wa jamii ya Bukusu.
Sinino anasema wapashaji tohara wamepuuzwa kaunti ya Bungoma jambo ambalo ansema huenda likapelea utamaduni huo ukapotea akitahadharisha wapashaji tohara wa kitamaduni kutopasha watoto tohara akisema atakayepatikana ataadhibiwa.
2.
MSAADA WA CHAKULA WATOLEWA KWA WAATHIRIWA WA MAFURIKO WEBUYE MASHARIKI
Waathiriwa wa janga la mafuriko na Korona katika wadi ya Sitikho eneo bunge la Webuye mashariki wamenufaika na chakula kutoka kwa wahisani eneo hilo kama njia mojawapo ya kuwanusuru wakti huu wanapopitia hali ngumu ya maisha.
Wakizungumza na wanahabri baada ya kuzuru maeneo mbalimbali ya eneo hilo ikiwemo Mukite,Khalumuli na Sitikho,wahisani hao wakiongozwa na Joseph Munyasia wamesema kuwa kuwa wameamua kuchukua hatua hiyo ya kusaidia jamii za eneo hilo kutokana na hali ngumu zinazopitia hasa wakti huu wa janga la Korona na mafuriko.
Kwa upande wao waathiriwa walionufaika na msaada huo wamepongeza familia ya munyasia kwa msaada huo huku wakitoa wito kwa serikali kujitokeza na kuwapa msaada zaidi
Kwa upande wao viongozi wa utawala wa eneo hilo wakiongozwa na chifu wa kata ya sitikho David manali na naibu wake John Murutu wameahidi kushirikiana na wakaazi wa eneo hilo kuhakikisha kuwa wananufaika na msaada kutoka kwa serikali pamoja na wahisani huku wakiwataka kuzingatia maagizo ya wizara ya afya ikiwemo kunawa mikono na kuvalia barakoa.
5
KHALWALE ATAKA SERIKALI KUU KUSITISHA SHUGHULI YA KUWAHAMISHA WAKAAZI WA MITAA YA RUAI NA KARIOBANGI
Aliyekuwa seneta wa kakamega dkt. boni khalwale ameitaka serikali kuu kusitisha mpango wa kubomoa makaazi ya wananchi katika mitaa ya ruai na kariobangi wakati huu mgumu wa janga la corona na mafuriko.
Akiongea wakati wa kuendeleza mpango wake wa ugavi wa chakula kwa waathiriwa wa mafuriko eneo bunge la mumias magharibi, khalwale amesema wamiliki wa ardhi hizo walizinunua kwa uhalali kutoka kwa serikali kupitia kwa aliyekuwa gavana wa nairobi evans kidero.
Aidha amemtaka rais uhuru kenyatta kutumia pesa anazopokea kama msaada wa kukabili janga la corona na mafuriko kuwafaidi waathiriwa husika, sawa na kuwapa wakenya mahitaji muhimu wakati huu wa kafyu.
3.
WAHUDUMU WA AFYA VIJIJINI WAPOKEA MSAADA WA BARAKOA
wahudumu wa afya nyanjani katika kaunti ndogo ya butere wamenufaika na msaada wa barakoa kutoka kwa aliyekuwa mbunge wa butere andrew toboso huku wakitoa wito kwa serikali kuwakumbuka katika utoaji wa vifaa vya kazi
Wakiongozwa na mwenyekiti wao martin shiboka na joel asumwa wameshukuru msaada wa toboso huku wakilalama kuwa kazi yao inawaweka katika hatari ya kupata maambukizo na ni muhimu serikali izingatie kuwapa vifaa na marupurupu ya kuwakimu
Aidha kupitia kwa mkubwa wao wametaja wizi vijijini kama changamoto miongoni mwao wakitaka serikali kuangazia jambo hilo
Sospeter omala kutoka afisi ya andrew toboso amesema kando na barakoa hizo, wanaendelea na mpango wa kuwapa chakula wenye changamoto katika jamii na amewahimiza viongozi kjitokeza kuunga mkono juhudi za toboso kuwasaidia wakazi kukabili corona
4
JAMAA AKAMATWA NA MAAFISA WA POLISI KAUNTI YA KAKAMEGA KWA KUSHIKIWA KUSAFIRI KUTOKA NCHINI TANZANIA
Maafisa wa usalama wakishirikiana na wale wa Afya kaunti ya Kakamega wanamzuilia mwanamume mmoja kutoka kijiji cha Shitoto wadi ya Butsotso mashariki eneo bunge la Lurambi baada ya kufika nyumbani kwake usiku baada ya kusafiri kutoka nchi jirani ya Tanzania alipokuwa akifanya kazi.
Kulingana na chifu wa Butsotso mashariki Justus Mukoshi ambaye akiandamana na maafisa hao anasema kuwa alipata ripoti kutoka Kwa wanakijiji kuwasili Kwa mwanaume huyo Kwa jina Philip Vincent Anzsla kutoka nchi jirani ya Tanzania kabla ya kuelekea nyumbani kwake.
Hata hivyo chifu huyo anasema kuwa baada ya kumchukua mshukiwa huyo iliwabidi pia kuwazuia nyumbani watu sita wa familia yake akiwemo mkewe na watoto ambao alikuwa ametengamana nao Kwa muda wa siku kumi na nne.
6
WAKAAZI WALALAMIKA KUHUSU HUDMA DUNI ZA HOSPITALI YA RUFAA YA KAKAMEGA
17TH MAY 2020
18;46
Baadhi ya wakazi wa kaunti ya kakamega wamelalamikia huduma duni katika hospitali ya rufaa ya kakamega huku wakimtaka gavana Wycliffe Oparanya kuchukua hatua ya kuzuru hospitali hiyo kurekebisha hali yake
Mama Julia inyambula kutoka lurambi ambaye anauguza mzee wake analalama kuwa licha ya mzee wake kupatikana kuwa na ugonjwa wa saratani, hakuna usaidizi wowote wa matibabu ambao anapokea kila anapoizuru, hospitali hiyo
Wakazi wanamtaka gavana Oparanya kufanya ziara ya ghafla katika hospitali hiyo na kujionea namna wananchi wanahangaika bila kupata huduma kwenye hospitali hiyo ya Kakamega ambayo walijivunia ilipoidhinishwa kuwa ya rufaa
7 WABUNGE NA VIONGOZI KUTOKA MAGHARIBI WAPANGA KUJADILI MUELEKEO WA KISIASA KABLA YA KURA YA MAAMUZI KUBADILI KATIBA
Siku moja tu baada ya kubainika kuwa mpango wa kuandaa kura ya maamuzi ya marekebisho ya katiba tayari imechapishwa kwenye gazeti rasmi la serikali, sasa wabunge kutoka eneo la magharibi wanapanga kukutana ili kuafikiana mwelekeo wa kisiasa ambao watachukua.
Mbunge wa ikolomani benard shinali ambaye pia ndio mwenyekiti wa wabunge wa kaunti ya kakamega, amesema kwa muda mrefu eneo hilo limekuwa likitengwa katika nafasi za uongozi serikalini, na kuwa wakati huu wanataka wawe mstari wa mbele kujadili masuala ya kitaifa kabla ya uchaguzi mkuu wa 2022.
Akiongea na waandishi wa habari alipokuwa akipeana chakula kwa watu wasiojiweza huko ikolomani, shinali aidha ameitaka serikali kuwahusisha viongozi katika mipango yake ya kuwasaidia wanaoathirika na njaa wakati huu ambapo wanasakamwa na hali ngumu ya maisha.
8
SERIKALI YAPANGA KUHAMISHA WALIOATHIRIKA NA MAFURIKO
Serikali kuu imeanzisha mpango wa kuwahamisha wakaàzi wa wanaoishi kando ya mito na hii ni kufuatia maafa yanayoshuhudiwa kila mara mito hiyo inapofurika na kuvunja kingo zake
Hata hivyo asilimia kubwa ya wakaazi hao huenda wakaachwa nje ya mpango huo kutokana na ukosefu wa stakabadhi za kumiliki shamba ambazo ni muhimu katika shughuli ya kuwahamisha.
Kulingana na wenyeji, wengi wao wamekuwa wakiridhi mashamba kutoka kwa babu zao hali ambayo imepelekea wengi wao kukosa stakabadhi za kuridhi shamba
Ni jambo ambalo limemlazimu mbunge wa eneo hilo christopher aseka..kuingilia kati ili kuwasaidia wenyeji kupata stakabadhi za umiliki ili waweze kuhamishwa hadi sehemu salama
NATIONAL NEWS